NAFASI YA ITIKADI KISIASA KATIKA MUSTAKABALI WA TAIFA
Mustakabali wa taifa unategemea sana utendaji wa wanataifa na wadau wao katika sekta mbali mbali za kiuchumi na za kiutamaduni. Utendaji nao kwa namna moja ama nyingine unaathiriwa na sera za nchi katika sekta hizo. Wakati sera za kiuchumi uathiri shughuli za kiuchumi zinavyoendeshwa katika nchi, kitu gani kinazalisha na kutumiwa na nani, na ni nani anashikiria njia gani ya uchumi, sera za masuala ya jamii huiongoza jamii katika taratibu za maisha ya siku kwa siku. Kadhalika katika utawala ni sera za kiutawala zinazotoa mwongozo.
Hatua ya kutunga na kurasmisha sera ni muhimu sana. Kutungwa kwa sera nako kunategemea nguvu za kisiasa ziko mikononi mwa nani na zinatumikaje. Aidha hatua ya kuamua nani awe na nguvu za kisiasa yaweza kutegemea sana itikadi iliyopo.
Kwa mantiki hiyo, itikadi ya nchi au jumuiya fulani ndio kiini cha nguvu za kisiasa, cha sera, cha utendaji na cha mustakabali wa taifa.
Hivyo, ni muhimu sana kuwa na itikadi iliyo njema ili mustakabali wa taifa uwe mwema pia.
Lakini itikadi ni sehemu tu ya siasa ya kundi husika. Katika ainisho, siasa ni njia za kutafuta na kupata nguvu, na vile vile ni njia anazozitumia/wanazozitumia mwenye/wenye nguvu katika kuhakikisha anabaki/wanabaki na nguvu hizo hususan za kiutawala ili afanye/ wafanye mazuri/mabaya kwa taifa/jamii kutegemeana na msukumo alionao/walionao. Kadhalika siasa ni kuamini kwamba njia fulani fulani zinawezesha ufikiaji wa malengo fulani. Lakini kama ulivyo msemo wa kibusara, imani sharti iambatane na matendo, vinginevyo si imani kamili.
Kwa mantiki hiyo siasa ina uwili/udaikotomi, yaani imani(itikadi) na mchakato wa utendaji.
Kwa maneno mengine, kuna ngazi mbili zinazoweza kulipeleka taifa katika mustakabali mwema. Ngazi ya kwanza ni siasa katika itikadi, wakati ngazi ya pili ni siasa katika mchakato.
Siasa katika mchakato, imegawanyika zaidi katika sehemu tatu, yaani maamuzi kwa kutegemea zilipo nguvu za kisiasa, utekelezaji utokanao na sera zilizopo za kiutawala, kiuchumi na kijamii. Hatimaye sehemu ya tatu ya mchakato ni matokeo.
Nayo sehemu ya maamuzi inategemea nguvu za kisiasa ziko mikononi mwa nani. Nguvu za fulani fulani za kisiasa zinaweza kuwa mikononi mwa mtu mmoja mmoja (individuals), au mikononi mwa wateule wa daraja fulani la juu katika jamii (elites) au katika vyama (parties) na au mikononi mwa watu(demos). Hapo ndipo panapoibuka dhana za aristokrasia, demokrasia, demokrasia ya vyama vingi, demokrasia huru, na dhana nyinginezo.
Palipo na nguvu ndipo palipo na maamuzi na ndipo palipo na maelekezo ya kitu gani kitekelezwe kitu gani kiachwe. Maamuzi na maagizo ndizo sera. Hivyo chimbuko na aina ya sera ni nguvu ziko mikononi mwa nani.
Kutoka nguvu ziliko tunapata sera za kiutawala. Ni sera hizi ambazo hutafsiriwa katika madaraka yaliyomo katika mihimili ya dola, hususan muundo wa serikali. Matharani, sera za kiutawala zaweza kuwa serikali kuundwa na chama kinachoshinda uchaguzi, serikali kuwa ya umoja wa kitaifa, madaraka serikali kuu (centralization), madaraka mikoani (decentralization)
Sera za kiuchumi huangilia masuala ya raslimali kuanzia mitaji fedha, nguvu kazi au suala zima la raslimaliwatu, na hadi rasilimali maliasili.
Katika sera kijamii kuna masuala ya utamaduni na huduma za jamii. Huduma za jamii ni pamoja na elimu, afya, ulinzi, usafiri na kadhalika.
Sera hizi katika mgawanyiko wake, zijapo pamoja katika kizitekeleza, ndizo huzalisha kiwango cha ustawi wa jamii husika, yaani mustakabali wa taifa/ jamii.

0 comments:
Post a Comment